Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuna viumbe millioni 8.7 duniani sasa:UNEP

Kuna viumbe millioni 8.7 duniani sasa:UNEP

Utafiti mpya uliofanywa na shirika la Umoja wa mataifa la mazingira UNEP kuhusu sensa ya viumbe duniani umebaini kuwa kuna vimbe milioni nane na laki saba vinavyoishi duniani hivi sasa.

Utafiti huo ni wa kwanza kutolewa hasa kwa kutanabaisha takwimu. Utafiti huo uliofanywa na UNEP unasema viumbe milioni 6.5 viko nchi kavu na milioni 2.2 vinapatikana majini. Utafiti huo pia umeonyesha kwamba asilimia 86 ya viumbe vyote vya nchi kavu na asilimi 91 ya vile vya majini bado havijabainishwa kwenye vitabu au majarida. George Njogopa anaripoti.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)