Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vikwazo vya Israel vinadumiza uchumi Palestina:UNCTAD

Vikwazo vya Israel vinadumiza uchumi Palestina:UNCTAD

Ukuaji wa uchumi katika maeneo ya Wapalestina yanayokaliwa umeonyesha kuimarika kwa mwaka 2010, ingawa ukosefu wa ajira, umasikini na matatizo ya chakula vinaendelea kwa kiwango cha juu umesema mpango wa Umoja wa mataifa wa biashara na maendeleo UNCTAD.

Mwaka jana uchumi umekuwa kwa asilimia 9.3 lakini ulichagizwa na msaada kutoka kwa wahisani kuliko uzalishaji katika maeneo hayo. UNCTAD inasema vikwazo dhidi ya uingizaji wa mali ghafi unadumaza ukuaji wa sekta binafsi na uwekezaji katika mindombinu. Pia vikwazo vilivyowekwa na Israel katika kuingiza na kutoa bidhaa Gaza na Ukingo wa Magharibi vimezuia maendeleo ya sekta ya nje ambayo inaweza kuchangia maendeleo ya uchumi. Mahmod Elkhafif ni mratibu wa UNCTAD wa misaada kwa watu wa Palestina.

(SAUTI YA MAHMOUD ELKHAFIF)

Tatizo la ajira Palestina ni miongoni mwa yanayoongoza duniani ikiwa na asilimia 50 ya vijana wa chini ya umri wa miaka 30 hawawezi kupata kazi.