Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wa kuomba msaada kwa ajili ya pembe ya Afrika kufanyika Addis Ababa

Mkutano wa kuomba msaada kwa ajili ya pembe ya Afrika kufanyika Addis Ababa

Mkutano wa Kimataifa ulioandaliwa na Umoja wa Afrika kwa ajili ya kuomba msaada wa kukabiliana na matatizo yanayoikabili pembe ya Afrika hivi sasa utafanyika kesho Alhamisi mjini Addis Ababa Ethiopia.

Lengo la mkutano huo ni kuonyesha mshikamano kwa waathirika wa ukame na njaa kwenye pembe ya Afrika, na Umoja wa Afrika umeziomba nchi wanachama kukusanya fedha zitakazosaidia kuokoa maisha ya mamilioni ya watu wanaohitaji msaada wa dharura hivi sasa hususani Somalia, Ethiopia, Djibouti na Kenya.

Mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa, ya kitaifa, kimataifa na yasiyo ya kiserikali yanaendelea na juhudi za kutoa msaada lakini bado fedha zinahitajika kukidhi mahitaji.

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Asha Rose Migiro atakwenda na ujumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa kwenye mkutano huo kama alivyomfahamisha Flora Nducha.

(MAHOJIANO NA ASHA ROSE MIGIRO)