Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Juhudi za kuokoa maisha zinaendelea pembe ya Afrika

Juhudi za kuokoa maisha zinaendelea pembe ya Afrika

Nchini Ethiopia shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limepeleka timu ya dharura kwenye eneo la Gode kilometa 250 Kaskazini mwa kambi ya wakimbizi ya Dollo Ado. Kwa ushirikiano na serikali ya Ethiopia, mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa na NGO’s, UNHCR inachukua hatua kukabiliana na wimbi kubwa la wakimbizi wapya 18,000 walioingia kutoka Somalia.

Timu hiyo inajumuisha wataalamu wa afya, lishe, ulinzi, uratibu na uandikishaji. Kazi yao kubwa ni kuweka kumbukumbu na kuandikisha wakimbizi wapya, kubaini mahitaji yao na kuwapa msaada. Na kukidhi mahitaji ya wakimbizi hao wapya UNHCR itahitaji kuingiza msaada kwa ndege kutoka Dubai kama anavyofafanua Adriane Edward msemaji wa UNHCR.

(SAUTI YA ADRIANE EDWARD)