Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mapigano yanayoendelea Tripoli ni kikwazo cha kusafirisha wahamiaji

Mapigano yanayoendelea Tripoli ni kikwazo cha kusafirisha wahamiaji

Hali bado ni tete kwenye mji mkuu wa Libya Tripoli huku kukiarifiwa mapigano makali baina ya waasi na majeshi ya serikali. Leo mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Libya Abdel Elah Al-Khatib na mshauri wa masuala ya Libya Ian Martin wanakutana mjini Doha Qatar na uongozi wa baraza la mpito la serikali ya Libya kujadili hali halisi.

Wakati huohuo mipango ya kuwahamisha mamia ya wafanyakazi wahamiaji waliokwama nchini Libya imesitishwa kutokana na mapigano yanayoendelea yaliyosababisha boti ya shirika la kimataifa la uhamiaji IOM kushindwa kutia nanga mjini Tripoli kama ilivyopangwa. IOM inasema ruksa ya kutia nanga iliyotolewa na baraza la mpito jana, leo imeifuta, shirika hilo lilipanga kuwasafirisha wahamiaji 300 waliokwama Tripoli. Jumbe Omari Jumbe kutoka IOM anafafanua.

(SAUTI YA JUMBE OMARI JUMBE)

Ameongeza kuwa kuna uwezekano wa kupeleka boti zingine mbili kusafirisha wahamiaji 2000 kutoka Tripoli punde usalama utakapoimarika.