Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la haki za binadamu laitaka Syria kusitisha ghasia

Baraza la haki za binadamu laitaka Syria kusitisha ghasia

Baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa litapeleka tume ya kimataifa ya uchunguzi nchini Syria kuuchunguza ukiukwaji wa haki za binadamu uliofanyika wakati wa kuwasaka waandamanaji wanaoipinga serikali . Wakati wa hitimisho la kikao maalum cha siku mbili kuhusu Syria baraza hilo limepitisha azimio ambalo linalaani vikali kuendelea kwa ukiukwaji wa haki za binadamu unaofanywa na serikali ya nchi hiyo.

Baraza limeitaka serikali ya Syria kusitisha mara moja mauaji, matumizi ya nguvu kupita kiasi, kuwaweka watu kizuizini, utesaji, uonevu na vitisho kwa wanaoandamana kwa amani. Wajumbe 33 wa baraza wamepiga kura kuunga mkono azimio hilo, huku wane wakiwemo Urusi, Uchina, Cuba na Ecuador wamelipinga. Cezary Lusinski ni mwakilishi wa Poland kwenye baraza la haki za binadamu.

(SAUTI YA CEZARY LUSINSKI)

Uchina na Urusi wamesema wanapinga azimio hilo kwani lina lengo la kuuondoa madarakani utawala halali, na halitoi fursa ya majadiliano na hivyo litatumika kuisambaratisha Syria.