Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu 600 wauwawa katika mapigano ya kikabila Kusini mwa Sudan

Watu 600 wauwawa katika mapigano ya kikabila Kusini mwa Sudan

Watu wapatao 600 wameripotiwa kuuwawa na kiasi kingine cha watu 700 kujeruhiwa kufuatia mapigano ya kikabila yaliyozuka huko Kusini mwa Sudan katika jimbo la Jonglei.

Kulingana na shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na ustawi wa Sudan UNMISS machafuko hayo yamezuka kuanzia alhamisi iliyopita. Jamii ya watu wa Murle na ile ya Lou-Nuer inazozana kuhusiana na mifugo. Maafisa wa Umoja wa Mataifa wamewasili kwenye eneo hilo la mzozo kwa ajili ya kufanya tathmini zaidi.