Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Waafiki kukusanya fedha ili kulinda kupotea kwa tembo barani Afrika

Waafiki kukusanya fedha ili kulinda kupotea kwa tembo barani Afrika

Mkutano uliwajumuisha wataalamu mbalimbali umemalizika huko Geneva, na kuafikia kutengwa kwa fungu la fedha kwa ajili ya kufadhilia miradi ya kuvilinda viumbe vilivyopo hatarini kutoweka . Mkutano huo uliofadhiliwa na Umoja wa Mataifa umeazimia kutenga fungu maalumu ili kusaidia kuwalinda wanyama jamii ya tembo walioko barani afrika ambao wapo hatarini kuadimika kutokana na wimbi la uwindaji haramu.

Chini ya makubaliano hayo, kumeazimia kutengwa kiasi cha dola za kimarekani milioni 100 katika kipindi cha miaka mitatu ijayo ili kusaidia marekebisho ya mifumo ya kiutendaji ikiwemo ile inayohusu miundo ya sheria. Wimbi la uwindaji haramu linaarifiwa kushika kasi barani Afrika na baadhi ya maeneo huko Asia.