Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uhusiano wa viumbe na mazingira ni muhimu kwa usalama wa chakula:UNEP

Uhusiano wa viumbe na mazingira ni muhimu kwa usalama wa chakula:UNEP

Kutambua mfumo bora wa mahuasiano ya viumbe na mazingira kwa ajili ya vyanzo vya maji na salama wa chakula kunaweza kusaidia kuzalisha zaidi chakula, kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa na kuleta faida kubwa za kiuchumi kwa jamii masikini.

Hayo yamo kwenye ripoti mpya iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira UNEP kwa ushirikiano na taasisi ya kimataifa ya udhibiti wa maji IWMI na mashirika mengine 19.

Ripoti inaonyesha jinsi gani ya kuangalia na kuwekeza kwenye uhusiano wa viumbe na mazingira, maji na chakula kupitia kilimo cha mazao mbalimbali, kupanda miti, kuboresha uvunaji wa maji ya mvua na hatua zingine kutasaidia kuepuka tatizo la maji na kutosheleza mahitaji ya chakula kwa idadi ya watu inayoongezeka kwa kasi duniani ambapo inakadiriwa kufikia bilioni 9 hapo 2050. George Njogopa anaripoti.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)