Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR imetoa wito wa usalama kwa raia wa kigeni Libya

UNHCR imetoa wito wa usalama kwa raia wa kigeni Libya

Kamishina mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR ametoa wito wa kuhakikisha usalama kwa raia wa kigeni nchini Libya.

Kamishina Antonio Gutetrres ametoa wito huo leo na kuziomba pande zote kwenye mgogoro wa Libya kuhakikisha kwamba maelfu ya raia wa kigeni waliokwama mjini Tripoli na maeneo mengine ambako mapigano yanaendelea kulindwa. Amesema wahamiaji na hususani kutoka Afrika wamekuwa na hofu kubwa hivi sasa.

Amesema ni muhimu kuhakikisha sheria za kimataifa za haki za binadamu zinazingatiwa na wahamiaji wakiwemo wakimbizi wanalindwa kikamilifu. Maelfu ya watu wakiwemo wahamiaji wamekimbia Libya tangu kuzuka kwa machafuko lakini bado kuna wengine wengi wanaaminika kusalia Tripoli na maeneo mengine.