Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Waasi wadhibiti mji mkuu wa Tripoli nchini Libya

Waasi wadhibiti mji mkuu wa Tripoli nchini Libya

Taarifa kutoka nchini Libya zinasema wapiganaji waasi wanaopinga utawala wa Rais Muammar Gaddafi hivi sasa wanaushikilia mji mkuu Tripoli baada ya majeshi ya serikali kusambaratika. Viongozi wa dunia wamekuwa wakitoa wito kwa Rais Gaddafi kuachia madaraka ili kunusuru maisha ya watu yanayoendelea kupotea kila siku. Wakati huohuo mwendesha mashitaka wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC Lui Moreno Ocampo amesema wamepokea taarifa za vyombo vya habari kuwa mtoto mkubwa wa kiume wa Rais Gaddafi Saif al-Islam anayetakiwa na mahakama hiyo amekamatwa, na imefanya mawasiliano na baraza la mpito la serikali ya Libya kuhusu hatima yake.

ICC inasema baraza hilo limeelezea juhudi za kutuliza hali nchini humo, kudhibiti usalama na mashambulizi dhidi ya raia. ICC imesema pia itafanya majadiliano ya kujisalimisha kwa bwana Islam katika mahakama hiyo kutokana na kibali cha kukamatwa kilichotolewa na mahakama hiyo tarehe 27 Juni mwaka huu. Kibali hicho kinamuhusu pia Rais Gaddafi, na Abdullah Al-Senussi ambao wanadaiwa kuhusika na uhalifu dhidi ya ubinadamu ikiwemo mauaji na utesaji. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon alikuwa na haya ya kusema kuhusu maendeleo ya hali nchini Libya.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)