Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM ni muhimu sana kwa kila jambo duniani:vijana

UM ni muhimu sana kwa kila jambo duniani:vijana

Mwezi huu mwaka wa kimataifa wa vijana umekamilika ambapo Umoja wa Mataifa kwa miezi 12 umekuwa ukipiga debe kuzitaka nchi wanachama kutoa nafasi kwa vijana kushiriki katika masuala muhimu yanayoisumbua dunia.

Na kwa vijana wenyewe Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekuwa na mikutano nao na kuwachagiza kuwa wakati wao umewadia kutatua matatizo yanayotikisa ulimwengu ikiwemo umasikini, uchumi, migogoro ya kisiasa, vita, njaa, mabadiliko ya hali ya hewa na amani. Na mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa yamekuwa yakitoa fursa kwa vijana kupata uzoefu hususani wanaosoma katika vyuo na kutambua umuhimu na kazi za Umoja wa Mataifa.

Vijana wawili kutoka Kenya na Tanzania ni miongoni mwa waliobahatika kupata uzoefu kwenye Umoja wa Mataifa wako nami hapa studio kujadili waliojifunza na fikra zao.

 (MJADALA NA VIJANA)