Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maafisa wa serikali ya Syria wapatao 50 watuhumiwa kupalilia mauwaji

Maafisa wa serikali ya Syria wapatao 50 watuhumiwa kupalilia mauwaji

Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa linaloangazia haki za binadamu Bi Navi Pillay amesema kuwa jumla ya watu 50 wanatuhumiwa kuwa nyuma ya uendeshaji wa vitendo vya mauwaji ya raia nchini Syria. Bi Pillay ametoa kauli hiyo kwa kuzingatia ripoti ya waaangalizi iliyofuatilia hali jumla ya mambo nchini humo ambako serikali imeendelea kuyadhibiti na kuyakandamiza makundi ya watu wanaoandamanaji.

Ripoti hiyo imesema kuwa kiasi cha watu 1,900 hadi sasa wameuwawa kufuatia operesheni inayoendeshwa na vikosi vya serikali kukandamiza maandamano hayo. Kulingana na Bi Pillay watu hao 50 waliotuhumiwa kwenye ripoti hiyo wanashikilia nyadhifa mbalimbali serikalini.