Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP inawasaidia waathirika wa mafuriko Bangladesh

WFP inawasaidia waathirika wa mafuriko Bangladesh

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP linatoa msaada wa dharura wa chakula unaohitajika kwa watu 57,000 walioathirika na mafuriko Kusini mwa Bangladesh. Shirika hilo linasema maefu ya familia masikini zimeathirika na mafuriko hayo ambayo pia yamewaacha wengi wakiwa wamekwama kwenye nyumba zao bila chakula na malazi.

Maeneo mengi ya wilaya ya Satkhira yamefunikwa na maji kutokana na mvua kubwa zinazonyesha kwa wiki mbili sasa. WFP inasema kutokana na fedha zilizotolewa na serikali ya Australia imeweza kusambaza tani 34.5 za biskuti kwa familia 11,500 ambazo ni jumla ya watu 57,000 wa wilaya hiyo.