Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maelfu ya wahamiaji bado wanahitaji kuhamishwa Libya:IOM

Maelfu ya wahamiaji bado wanahitaji kuhamishwa Libya:IOM

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM linafanya juhudi za kuendelea kuwahamisha maelfu ya wahamiaji wanaohitaji msaada kwenye mji mkuu wa Libya, Tripoli. Shirika hilo linasema limepokea maombi mengi ya kuwahamisha wahamiaji wa kigeni mjini Tripoli ambao wako katika hali mbaya na sasa wanataka kuondoka.

Idadi kubwa ya wahamiaji kutoka Misri bado wako Tripoli na Magharibi mwa Libya ikiwa ni pamoja na wahamiaji kutoka mataifa mengine yakiwemo ya Asia na Afrika. Idadi kamili ya wahamiaji haijulikani lakini maelfu ya Wamisri wamejiandikisha kwenye ubalozi wao na wako tayari kuondoka. IOM inasema kutokana na matatizo mengi ya kiufundi, kisiasa na changamoto za kisalama itahitahi fedha zaidi ili kutekeleza hatua hiyo haraka. Jumbe Omari Jumbe ni afisa habari na mawasiliano wa IOM.

(SAUTI YA JUMBE OMARI JUMBE)