Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Zingatio la usalama na usafi kwa viwanda vya nguo vya Cambodia bado liko chini-Ripoti ya UM

Zingatio la usalama na usafi kwa viwanda vya nguo vya Cambodia bado liko chini-Ripoti ya UM

wafanyakazi wa viwanda vya nguo Cambodia

Ripoti moja iliyotolewa na Umoja wa Mataifa imetaja kuwepo kwa baadhi ya vitendo vinavyohatarisha afya za watu kwenye viwanda vya uzalishaji nguo nchini Cambodia. Ripoti hiyo ambayo hata hivyo imeridhika na namna viwanda hivyo vinavyopiga hatua kuzingatia viwango vya kimataifa, imesema kuwa kwenye baadhi ya maeneo bado hali ya usalama ni ya kutia mashaka.

Imesema kwa mfano maeneo kama yanayohusu zingatio jumla la afya, bado halijapewa msukumo unaostahili jambo ambalo ni hatari kwa wafanyakazi. Vile vile imetaja vitendo kama unyanyapaa ambavyo imesema kuwa linakwaza ustawi wananchi wengi.