Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama lataka hatua zichukuliwe kwa waliotekeleza shambulizi la kigaidi Iraq

Baraza la Usalama lataka hatua zichukuliwe kwa waliotekeleza shambulizi la kigaidi Iraq

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo limelaani vikali mashambulizi ya kigaidi yaliyokatili maisha ya watu wengi nchini Iraq na kujeruhi wengine mapema wiki hii na kusisitiza kwamba wahusika lazima wafikishwe kwenye vyombo vya sheria.

Akisisitiza kuhusu hilo jambo balozi wa India kwenye Umoja wa Mataifa ambaye ndiye Rais wa wa baraza kwa mwezi huu Hardeep Singh Puri amesema kuna haja ya kuwafikisha wahusika, walioandaa na wanaofadhili vitendo hivi vya kikatili dhidi ya raia wa Iraq. Baraza la usalama limezitaka nchi zote wanachama chini ya maazimio ya baraza na wajibu wao wa kutekeleza sheria za kimataifa kushirikiana na uongozi wa Iraq kuwatafuta wahusika wa mashambulizi ya Jumatatu wiki hii. Kwa mujibu wa duru za habari kulikuwa na mashambulizi 37 katika zaidi ya miji 12 ikiwemo mabomu ya kutegwa kwenye magari na yale ya kujitoa muhanga, watu 80 waliuawa na zaidi ya 300 kujeruhiwa.