Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ofisi ya haki za binadamu ya UM yachapisha ripoti ya uchunguzi kuhusu Syria

Ofisi ya haki za binadamu ya UM yachapisha ripoti ya uchunguzi kuhusu Syria

Ofisi ya kamishina mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa leo Alhamisi imechapisha ripoti ya tume maalumu ya uchunguzi iliyokwenda Syria. Tume hiyo iliundwa na baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa wakati wa kikao maalum kuhusu Syria April 29 ili kuchunguza madai yote ya ukiukwaji wa sheria za kimataifa za haki za binadamu na kupata ukweli na mazingira ya madai ya ukiukwaji huo na uhalifu mwingine.

Kamati hiyo inasema imebaini ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu ambao unaweza kuwa ni uhalifu dhidi ya ubinadamu. Ukiukwaji huo unajumuisha mauaji na kutoweka kwa watu, wamebaini mauaji ya watu wakiwemo 353 ambao majina yao yamepatikana. Kwa jumla imepokea majina 1900 na taarifa za watu kuuawa Syria tangu Machi 2011. Rupert Colville ni msemaji wa ofisi ya haki za binadamu.

(SAUTI YA RUPERT COLVILLE)

Tume hiyo imependekeza kwamba baraza la usalama litafakari kuipeleka hali ya Syria kwenye mahakama ya kimataifa ya uhalifu ya ICC.