Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM utaendelea kusaidia Somalia kusaka amani ya kudumu:Mahiga

UM utaendelea kusaidia Somalia kusaka amani ya kudumu:Mahiga

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Balozi Augustine Mahiga amewaambia wajumbe wa baraza la amani na usalama la Umoja wa Afrika mjini Addis Ababa nchini Ethiopia kuwa Umoja wa Mataifa utaendelea kuisaidia Somalia kuhakikisha inapata amani ya kudumu.

Mahiga amesema ofisi ya Umoja wa Mataifa ya masuala ya kisiasa kwa ajili ya Somalia UNPOS yenye makao yake mjini Nairobi, Kenya inatathimini mipango yake na inatarajia kupanua wigo wa uwemo wa Umoja wa Mataifa ndani ya Somalia, na hasa wafanyakazi wa kiraia wa Umoja wa Mataifa mjini Moghadishu, hata hivyo amesema jambohilo  litahitaji vikosi zaidi kwa ajili ya ulinzi. Mahiga amelieleza baraza hilo hatua kubwa zimepigwa katika mchakato wa amani ya Somalia ingawa juhudi zaidi bado zinahitajika na hasa katika masuala ya kiufundi, vifaa na fedha. Mkutano huo wa baraza la amani na usalama ulikuwa unajadili masuala makubwa matatu kama anavyofafanua balozi Mahiga.

(SAUTI YA BALOZI MAHIGA)