Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ivory Coast kuchukua hatua zaidi kuelekea utawala wa sheria:UM

Ivory Coast kuchukua hatua zaidi kuelekea utawala wa sheria:UM

Walinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini Ivory Coast UNOCI wameisaidia nchi hiyo kukarabati gereza kubwa mjini Abidjan baada ya kusalia tupu kufuatia machafuko ya baada ya uchaguzi mkuu hivi karibuni. Ukarabati huo ni katika juhudi za kuisaidia Ivory Coast kurejesha utawala wa sheria nchini humo.

Kwa mujibu wa afisa wa UNOCI Francoise Simard hatua hii ni muhimu sana kwa nchi hiyo na kufufua upya taasisi za kisheria, na ameipongeza serikali mpya ya Ivory Coast katika hafla maalumu ya ufunguzi wa gereza hilo. George Njogopa ana taarifa kamili.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)