Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Muongozo mpya wa UM unalengo la kuimarisha msaada wa kisaokolojia kwa waathirika wa majanga

Muongozo mpya wa UM unalengo la kuimarisha msaada wa kisaokolojia kwa waathirika wa majanga

Shirika la afya duniani WHO na washirika wake wamezindua kitabu cha muongozo mpya kuwasaidia wafanyakazi katika maeneo mbalimbali kutoa msaada muhimu wa kisaikolojia kwa watu walioathirika na majanga na hali za dharura. Kwa mujibu wa WHO katika miaka mitano iliyopita athari za kisaikolojia zilizosababishwa na tsunami, matetemeko ya ardhi, ukame na vita zimedhihirisha kuwa ni mbaya zaidi kama athari za kimwili.

Shirika hilo limesema kwa kutambua hayo limeona haja ya kuongeza juhudi na kushughulikia afya ya akili kwa walioathirika na majanga, na ndio maana WHO na washirika wake wamezindua kitabu cha muongozo mpya ili kuhakikisha kwamba huduma muhimu na za kila mara zinapatikana kwa walioathirika.

Muongozo huo umetolewa kwenda sambamba na siku ya wahisani duniani inayoadhimishwa kila mwaka Agosti 19 ambayo hutambua mchango na kujitolea kwa wale wanaoweka maisha yao hatarini ili kuokoa ya wengine na kuwapa matumaini. Muongozo huo umetolewa kwa ushirikiano wa WHO, World Trauma Foundation na shirika la World Vision.