Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UN-HABITAT yazawadia vikundi vya vijana 59

UN-HABITAT yazawadia vikundi vya vijana 59

Ikiingia mwaka wake wa 3 tangu kuanza kutoa tuzo zinazochochea ukuaji wa kiustawi katika maeneo ya mijini, shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na makazi UN-HABITAT limevizawadia vikundi kadhaa ambavyo vimepiga hatua kwenye uboreshaji makazi. Vikundi hivyo 59 ambavyo vinaundwa na vijana vinatajwa kupiga hatua kwenye endelezaji wa miradi inayochochea makazi bora na utengamano wa kijamii.

Vikundi hivyo ni kutoka nchi 43 ambavyo vimefanikiwa kupata mafungu ya fedha baada ya kuainisha vyema miradi na matarajio kuhusiana na uboreshaji wa makazi na ustawi wa kijamii. Mfumo wa utoaji mafungo ya fedha kwa kupitia miradi ya uchambuzi ulianzishwa rasmi mwaka 2011