Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mamia ya watu wapya wawasili Italia kutoka Libya na Tunisia

Mamia ya watu wapya wawasili Italia kutoka Libya na Tunisia

Watu takribani 2000 wamewasili kwenye kisiwa cha Lampedusa nchini Italia wakitokea Libya na Tunisia limesema shirika la kuhudumia wakimbizi UNHCR. Watu 1800 kati yao wanasemekana kutoka eneo la Janzor kilometa 12 magharibi mwa mji mkuu wa Libya Tripoli ambako walisubiri kwa zaidi ya wiki moja hali ya bahari itulie kabla ya kuanza safari. Miongoni mwa watu hao 2000 kulikuwa na wanawake 200 na watoto 30. George Njogopa anaripoti.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)