Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa OCHA ataka msaada uongezwe Somalia

Mkuu wa OCHA ataka msaada uongezwe Somalia

Mratibu mkuu wa masuala ya kibinadamu na ya dharura wa Umoja wa Mataifa OCHA Valarie Amos ametoa wito wa kongeza msaada zaidi kwa ajili ya mamilioni ya Wasomali wanaokabiliwa na njaa.

Bi Amos ambaye amehitimisha ziara ya siku tatu nchini Somalia na Kenya amesema bado Wasomali wanakimbilia nchi jirani ya Kenya, watoto wanakabiliwa na utapia mlo na kambi ya wakimbizi ya Dadaab inayowapokea imefrika.

Ameitaka jumuiya ya kimataifa na wahisani kuongeza msaada zaidi kunusuru maisha ya mamilioni ya Wasomalia. Rita Maingi msemaji wa OCHA Kenya nafafanua kuhusu ziara hiyo ya siku tat ya Bi Amos.

(MAKALA OCHA)