Ban alaani vikali mashambulizi ya mabomu Iraq

15 Agosti 2011

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelaani vikali mlolongo wa mashambulizi ya mabomu katika miji kadhaa nchini Iraq yaliyofanywa hii leo kuuwa watu zaidi ya 70 na kujeruhi wengine wengi.

Ban amesema hivyo ni vitendo vya kinyama hasa kwa mashambulizi haya ktokea wakati wa mwezi mtukuf wa Ramadhan. Katibu Mkuu wamewataka watu wa Iraq kupinga majaribio yoyote ya kuchochea ghasia nchini humo.

Amezitolea wito pande zote za viongozi wa kisiasa nchini humo kuushirikiana na kufanya kazi pamoja kufikia amani ya kudumu kwa njia ya majadiliano na maridhiano.

Ametuma salamu za rambirambi kwa familia za waliopoteza maisha kwenye shambulio hilo na kuwatakia nafuu ya haraka majeruhi.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter