Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Shughuli za utoaji misaada zarejea tena Gaza

Shughuli za utoaji misaada zarejea tena Gaza

Shughuli za utaoji wa misaada ya kibinadamu zimerejea upya katika eneo la ukanda wa Gaza, na tayari afisa wa Umoja wa Mataifa amekaribisha hatua hiyo akisema kuwa sasa hatua hiyo ni nukta muhimu hasa panapohusika na ustawi wa jamii. Kulingana na duru kwenye eneo hilo, shirika la kimataifa lisilolo la serikali linalojihusisha na misaada ya kitabibu limerejea upya na kuendesha shughuli zake.

Kurejea upya wa shirika hilo kunakuja katika kipindi cha wiki moja baada ya kundi la Hamasa na Palestina kulipiga marafuku. Afisa wa Umoja wa Mataifa anayehusika na masuala ya mashariki ya kati Robert Serry amepongeza hatua hiyo akisema kuwa ni muhimu kwa ajili ya ustawi wa wananchi wa eneo hilo.