Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkataba wapitishwa kulinda bahari ya Caspian kutokana na mafuta:UNEP

Mkataba wapitishwa kulinda bahari ya Caspian kutokana na mafuta:UNEP

Nchi tano zinazopakana na bahari ya Caspian zimekuabaliana kuimarisha hatua mpya za pamoja za kikanda za kukabiliana na kuvuja kwa mafuta na kuboresha njia za kuangalia vyanzo vya uchaguzi wa mazingira miongoni mwa nchi hizo na mipaka yake.

Muafaka huo ulipitishwa wakati wa mkutano wa ngazi ya juu wa wawakilishi wa serikali za Azerbaijan, Iran, Urusi, Kazakhstan na Tarkmenistan walipokutana mjini Aktau Kazakhstan wiki iliyopita kwa mkutano wa wa tatu wa COP3 wa utekelezaji wa mkataba wa Tehran.

Makubaliano hayo ni ya kisheria yaliyotiwa saini na nchi zote tano za Caspian ili kulinda mazingira mkataba unaosimamiwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kulinda mazingira UNEP. Kama chanzo muhimu cha mafuta na gesi eneo la Caspian limekuwa likitupiwa macho kwa maswala ya kichumi na kisiasa katika miaka ya karibuni.

Kwa mujibu wa UNEP licha ya utajiri ambao unaletwa na mafuta katika eneo hilo , utajiri huo unaambatana na tishio kubwa la uchafuzi wa mazingira katika bahari ya Caspian. Safari 10,000 zinafanyika kila mwaka kusafirisha mafuta na bidhaa zingine za mafuta katika bahari ya Caspian.