Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Huu ni wakati wenu vijana kutatua matatizo ya dunia:M

Huu ni wakati wenu vijana kutatua matatizo ya dunia:M

Ijumaa hii Agosti 12 Umoja wa Mataifa na dunia kwa ujumla wameadhimisha siku ya kimataifa ya vijana kwa kauli mbiu “Badili dunia yetu” wito mahsusi kuwachagiza vijana kjitoa kimasomaso kushiriki masuala yahusyo maendeleo ya jamii zao.

Ikiwa pia ni siku ya mwisho wa mwaka wa Umoja wa Mataifa wa vijana Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon akiwa mjini Seoul Korea Kusini alikohudhuria mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mfano yaani UN Model amewasisitiza vijana kuwa huu ni wakati wao kusaidia kupata suluhu ya umasikini, matatizo ya ajira, mabadiliko ya hali ya hewa, maradhi , elimu, njaa na na changamoto zingine kwani wao ndio viongozi wa kesho. Ili kupata thaimini ya vijana wenyewe kuhusu siku hii na mchango wao katika jamii nimefanya mjadala na vijana kutoka Tanzania, Kenya na Rwanda ambao ni wanafunzi wa chuo kikuu cha kimataifa cha Kimarekani kilichoko Nairobi Kenya USIU ambao pia ni wanachama wa muungano wa vijana kwa ajili ya uongozi na maendeleo Afrika YALDER. Pia utawasikia vijana kutoka Burundi. Tuanze na vijana walioko Kenya

(MJADALA NA WANAFUNZI WA USIU)

Ushiriki wa vijana umekuwa ukitafsiriwa kwa namna mbalimbali hasa ukizingatia kuwa changamoto zinazowakabili ni nyingi  kubwa ni ajira kama alivyobaini mwandishi wetu ramadhani Kibuga alipozungumza na vijana mbalimbali mjini Bujumbura.

(MAONI VIJANA BURNDI)

Kurasa mpya kwa vijana umefunguliwa na nguvu ya vijana imedhihirika hasa Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini ambao vijana wameweza kun’goa madarakani tawala za kidikteta. Vijana hawa wanatoa wito gani kwa wenzao katika siku hii?

(WITO VIJANA)