Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakimbizi wa Afghanistan, Iraq walioko Iran wapatiwa bima ya afya

Wakimbizi wa Afghanistan, Iraq walioko Iran wapatiwa bima ya afya

Mpango unaoungwa mkono na Umoja wa Mataifa unatazamiwa kuwafaidia jumla ya wakimbizi milioni moja kutoka nchi za Afghanistan na Iraq ambao wanaishi huko Iran.Chini ya mpango huo mpya, wakimbizi hao sasa wanatazamiwa kupata bima ya afya ambayo itawasaidia kugharamia huduma za matibabu.

Hata hivyo shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR,limesema litaongeza ufadhili wake hadi kufikia asilimia 100 kwa wakimbizi ambao hawajiwezi kwa lolote.Kabla ya kufikiwa kwa mpango huo, wakimbizi hao walipewa ufadhili mmoja tu ule unaohusiana na kushindwa kufanya kazi kwa figo.