Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Askari wa UNAMID wazidi kushambuliwa- Gambari

Askari wa UNAMID wazidi kushambuliwa- Gambari

Vikosi vya kulinda amani vya kimataifa vinavyoendesha opereshani zake kwenye jimbo lenye mzozo Darfur wameendelea kuandamwa na matukio ya mashambulizi .Kulingana na Mkuu wa vikosi hivyo ambavyo muungano wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika UNAMID, Bwana Ibrahim Gambari amesema kuwa askari kadhaa wamepoteza maisha baada ya kushambuliwa na makundi korofi.

Amesema katika kipindi cha miezi mine iliyopita, askari watatu walipoteza maisha katika matukio tofauti.Bwana Ibrahim Gambari hivi karibu alilazimika kukutana na serikali ya Sudan ili kujadilia hali hiyo .