Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Deiss azungumzia chumi wa kimataifa nchini Argentina

Deiss azungumzia chumi wa kimataifa nchini Argentina

Udhibiti wa uchumi, utandawazi na jukumu la Umoja wa Mataifa ndio mada zilizotawala katika ziara ya sik moja ya Rais wa baraza la Umoja wa Mataifa Josef Deiss nchini Argentina.

Akiwa mjini Buenos Aires Jumatano bwana deiss amekutana na waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo Héctor Timerman, watunga sheria bungeni, wanadiplomasia vijana na mratibu wa Umoja wa Mataifa nchini humo. George Njogopa anaripoti.