Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Assad amepoteza uhalali wake asema balozi wa marekani UM

Assad amepoteza uhalali wake asema balozi wa marekani UM

Marekani inataka kwepo na vikwazo zaidi ili kusitisha machafuko nchini Syria. Balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa Susan Rice akizungumza na waandishi wa habari mjini NewYork ameyaelezea machafuko na ghasia dhidi ya raia nchini Syria ni kama vitendo vya kutisha. Bi Rice amesema anatiwa moyo na kauli za kimataifa za kulaani hali ya Syria akitaja baraza la usalama na pia taarifa iliyotolewa na Umoja wa nchi za Kiarabu Arab League. Ameongeza kuwa Marekani itaendelea kufanya kazi kwa karibu na washirika wake wa kimataifa ili kuongeza shinikizo.

(SAUTI YA SUSAN RICE)

Naye kamishina mkuu wa haki za binadamu Navi Pillay anatarajiwa kutoa taarifa kwenye baraza la usalama katika siku chache zijazo kuhusu hali nzima ya Syria.