Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban amezitaka pande husika kuhakikisha suluhu ya kisiasa ya mgogoro wa Libya

Ban amezitaka pande husika kuhakikisha suluhu ya kisiasa ya mgogoro wa Libya

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amezungumza kwa njia ya simu na waziri mkuu wa Libya Baghdadi al-Mahmudi Jumatano jioni.

Ban amefahamishwa kwamba baraza la salama limempa taarifa ya hali inayoendelea nchini Libya na limerejea kusisitiza masikitiko yake kuhsu kuendelea kupotea kwa maisha ya watu na kusambaratishwa kwa miundo mbinu.

Ban pia ameelezea hofu yake juu ya athari za mapigano kwa maisha ya raia na ukosefu wa madawa, huduma za afya na mafta suala linaloongeza msukumo wa msaada wa haraka wa kibinadamu  kwa maelfu ya watu wa Libya. Tofauti na taarifa zilizotolewa na vyombo vya habari vya Libya Katibu Mkuu hakuusema kama atalitaka baraza la usalama kuitisha kikao maalum.

Amemwambia waziri mkuu anasikitika kwamba hakuna hatua kubwa zilizopigwa katika juhudi za kufuatia suluhisho la kisiasa la mgogoro wa Libya kwa njia ya majadiliano licha ya jitihada kubwa za mwakilishi wake maalumu nchini humo, na amemtaka waziri mkuu kuchukua hatua madhubuti za mapendekezo ya mwakilishi maalumu wa UM nchini Libya.