Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Dunia lazima iisaidie Somalia katika kipindi hiki cha kihistoria kuelekea amani ya kudumu

Dunia lazima iisaidie Somalia katika kipindi hiki cha kihistoria kuelekea amani ya kudumu

Hatua zilizopigwa hivi karibuni kisiasa na kijeshi katika taifa la Somali lililoghubikwa na vita zinatoa fursa muhimu ya kupiga hatua na kukabiliana na changamoto zikiwemo wabbabe wa kivita na magaidi amesema leo afisa wa ngazi za juu wa Umoja wa Mataifa.

Balozi Augustine Mahiga ambaye ni mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa Somalia ameitolea wito jumuiya ya kimataifa kutoa misaada zaidi wa kifedha na kiufundi kusaidia taifa hilo lililosambaratika. Ameongeza kuwa huu ni wakati wa jumuiya ya kimataifa kuonyesha jukumu lake na kujitokeza kusaidia mchakato mzima na mara moja katika nyanja zote.

Wito huo ameutoa alipokuwa akitoa taarifa kwa baraza la usalama kwa njia ya video kwa mara ya kwanza kutoka mji mkuu wa Somalia, Mogadishu, amesema kwa kifupi Wasomali hawawezi kusubiri tena.

Mahiga amegusia kuwa hatua ya asilimia 95 ya wanamgambo wa Kiislamu wa Al-Shaababu kuondoka Mogadishu wiki iliyopita kutokana na shinikisho kutoka kwa vikosi vya kulinda amani vya muungano wa Africa AMISOM, na kuithinishwa kwa mukataba wa Kampala mwezi Julai na bunge la serikali ya mpito linalotoa mwaka mmoja zaidi kwa bunge hili lililotaka kujiongezea miaka mitatu.