Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tanzania yatakiwa kuchukua hatua baada ya utafiti wa ukatili dhidi ya watoto:UNICEF

Tanzania yatakiwa kuchukua hatua baada ya utafiti wa ukatili dhidi ya watoto:UNICEF

Umoja wa Mataifa umeichagiza serikali ya Tanzania kushughulikia haraka matatizo ya ukatili dhidi ya watoto baada ya matokeo ya utafiti uliofanywa na serikali ambapo zaidi ya robo tatu ya wasichana na wavulana wamesema wamekabiliwa ukatili na kuumizwa kimwili kabla ya kufikia umri wa miaka 18.

Kutokana na taarifa iliyotolewa leo na shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF matokeo hayo yanasema watoto wanatendewa ukatili ama na watu wazima kwenye familia au wenzi wao. Imeongeza kuwa karibu wasichana watatu kati ya 10 na mvulana mmoja kati ya saba  nchiniTanzania bara na visiwani wamesema wamefanyiwa ukatili wa kimapenzi.

Utafiti huo pia umebaini kwamba asilimia 25 ya watoto waliohojiwa wameshawahi kunyanyawa kihisia wakati wakikuwa. Utafiti huo umeongozwa na serikali na ulianza kufanyika 2009.