Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wachezaji nyota wa Barcelona wawatia moyo vijana

Wachezaji nyota wa Barcelona wawatia moyo vijana

Wanasoka wa kilabu ya FC Barcelona ya nchini Hispania ambao wanaunga mkono juhudi zinazochukuliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF wamejitokeza hadharani kuwapa moyo watoto wakisema kuwa wanaweza kufika mbali kama wataweka mapenzi yao kwenye soka.

Nyota hao wa dimba David Villa na Thiago Alcántara walijitokeza huko Dallas Marekani na kuwapa moyo wa matumaini vijana wa Afrika ambao wanandoto ya kusuma gozi hapo baadaye. Wamewaambia vijana hao kama wataendelea kuwa na mapenzi na ushawishi ndani ya soka, basi nao pia wanaweza kufikia nafasi hiyo. Pia walitumia fursa hiyo kuwapa matumaini ya pekee wakisema kuwa bado wapo kwenye ramani sahihi kufikia kwenye kilele cha mafanikio.