Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la usalama lalani vikali mashambulizi kwa askari wa UNAMID Darfur

Baraza la usalama lalani vikali mashambulizi kwa askari wa UNAMID Darfur

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limelaani vikali tukio la mashambuli yaliyowalenga vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika UNAMID vinavyoendesha operesheni zake katika jimbo la Darfur nchini Sudan, ambako  askari mmoja raia wa Sierra Leone alifariki dunia na wengine kadhaa kujeruhiwa.

Katika taarifa yake juu ya kadhia hiyo, baraza hilo limeitaka serikali ya Sudan watendaji wa jinai hizo wanafikishwa kwenye mkono wa haki. Aidha limerejea hatua yake kwa kusema kuwa litaendelea kutoa ushirikiano wa dhati kwa vikosi vyake hivyo vinachukua askari 23,000 ili kufanikisha utulivu wa amani kwenye eneo hilo. Tangu kuanza kwa mkwamo wa amani kwenye eneo hilo mwaka 2003, zaidi ya watu 300,000 wamepoteza maisha huku wengine milioni 2.7 wakilazimika kwenda uhamishoni.