Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Dk.Migiro azindua ripoti ya kupinga ukatili dhidi ya watoto Tanzania

Dk.Migiro azindua ripoti ya kupinga ukatili dhidi ya watoto Tanzania

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Asha Rose Migiro leo amezindua ripoti ya utokomezaji ya vitendo vya ukatili dhidi ya watoto nchini Tanzania. Uzinduzi huo ni utekelezaji wa azimio lililowekwa na Katibu Mkuu Ban Ki-moon mwaka 2006 alipozitaka nchi zote wanachaka kufanya utafiti wa kina ili kubaini miondo na mifumo ya unyanyasaji dhidi ya watoto.

Tanzania inakuwa nchi ya kwanza duniani kuendesha utafiti huo na kuzinduliwa rasmi ripoti yake. Ndani ya ripoti hiyo hata hivyo na taarifa za kusikitisha za watoto kudhulumiwa haki zao, kubakwa, kufanyishwa kazi ngumu na kutosikilizwa. Akizindua ripoti hiyo jijini Dar es salaam Bi Migiro amesema ili kuwa na taifa bora kesho lazima kuwekeza leo kwa watoto.

(SAUTI YA ASHA ROSE MIGIRO)