Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban akaribisha hatua zilizotangazwa na Marekani kusaidia kuzuia mauaji ya kimbari

Ban akaribisha hatua zilizotangazwa na Marekani kusaidia kuzuia mauaji ya kimbari

Juhudi zilizotangazwa na Rais Barack Obama wa Marekani hivi karibuni za kuimarisha uwezo wa serikali yake kusaidia kuzuia mauaji ya kimbari na unyama mwingine ni mipango inayotia matumaini amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon. Amesema ili jukumula la kuwalinda watu litekelezeke ipasavyo basi chi wanachama lazima wabuni mikakati mipya na kitekeleza kuanzia ngazi za kitaifa.

Amesema hivyo kuanzishwa kwa bodi maalumu ya ushirikiano kuzuia mauaji ya kimbari, hatua za kuwachukulia hatua wahusika na sera mpya za Marekani ni mambo yanayotia matumaini makubwa katika vita dhidi ya mauaji ya kimbari. Pia kuna mipango mingine ya kikanda inayoendelea Costa Rica, Denmark, Ghana, Argentina, Switzerland na Tanzania.