Afisa Mkuu wa vikosi vya kulinda amani amaliza muda wake na kutaja mafanikio

5 Agosti 2011

Afisa wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia  vikosi vya ulinzi wa amani Bwana Le Roy ambaye anajiandaa kumaliza muhula wake, amebainisha mafanikio yaliyofikiwa na idara hiyo na kusema kuwa kuna hatua kubwa zimepigwa ikiwemo utoaji ulinzi kwa mamia ya raia ulienda sambamba na utengamao katika mataifa kadhaa duniani.

Vikosi hivyo vya kulinda amani vimehudumu katika mataifa kadhaa kuanzia huko Liberia, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, mpaka Haiti, Timor–Leste. Kwa maana hiyo Bwa Re Roy anasema kuwa hayo ni mafanikio makubwa ambayo yanaainisha jukumu la kuwepo kwa vikosi vya ulinzi wa amani. Mkuu huyo alikuwa akizungumza na waandishi wa habari ikiwa ni mkutano wake wa mwisho kabla hajaondoka kwenye ofisi hiyo.

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter