Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sudan yachelewesha helkopta ya uaokoaji-UM

Sudan yachelewesha helkopta ya uaokoaji-UM

Mamlaka ya Sudan imetoa tishio kali la kutaka kuidungua helikopta itakayokwenda kwenye eneo la Abyei kwa ajili ya kutoa msaada wa kitabibu kwa askari wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa ambao wamejeruhiwa vibaya hatua ambayo imesababisha operesheni hiyo ya uokoaji kuchelewa kwa zaidi ya saa tatu.Hapo majuzi askari 3 wa Umoja wa Mataifa raia kutoka Ethiopia waliuwawa baada ya kulipukiwa na bomu la kutegwa ardhini na askari wengine 7 kujeruhiwa vibaya.

Vikosi vya Umoja wa Mataifa vimepelekwa kwenye eneo hilo la Abyei kwa shabaya ya kutekeleza ulinzi wa amani kufuatia kuzorota kwa amani katika siku za hivi karibu.Kulingana na Mkuu wa vikosi hivyo Bwana Le Roy amesema kuwa mamalaka ya Sudan ilitishia kuiangusha helikopta hiyo kama ingeruka pasipo kuruhusiwa.