Wataalamu wa UM waitaka Syria kutoendesha ghasia dhidi ya raia

5 Agosti 2011

Huku ghasia zinazoendeshwa na serikali ya Syria dhidi ya raia zikizidi kundi la wataalamu wa haki za binadam kutoka Umoja wa Mataifa wamerejelea wito  wao kutaka kusitishwa kwa ghasia hizo. Wito wa wataalamu hao unajiri baada ya baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kulaani ukiukaji wa haki za binadam unaoendelea nchini Syria na matuumizi ya nguvu dhidi ya raia kutoka kwa vikosi vya serikali.

Syria imeshuhudia ghasia tangu mwezi machi huku serikali ikitumia nguvu kuyazima maandamano hayo. Maandamano mengine yalishuhudiwa kaskazini mwa Afrika na mashariki ya kati tangu mwanzo wa mwaka huu na kuangusha serikali nchini Tunisia na Misri.

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter