Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama laani mauwaji ya askari wa kulinda amani Abyei

Baraza la Usalama laani mauwaji ya askari wa kulinda amani Abyei

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limelaani vikali juu ya kuuliwa kwa askari wa kulinda amani wanaohudumu katika jimbo lenye mzozo la Abyei,Sudan.Askari hao wanne walipoteza maisha baada ya kulipukiwa na bomu la kutengwa ardhini wakati wakiwa kwenye operesheni za ulinzi wa amani.Wote wa askari hao ni raia wa Ethiopia. Katika tukio hilo askari wengine saba walijeruhiwa.

Katika taarifa yake juu ya tukio hilo,Balozi wa India kwenye baraza hilo Hardeep Singh Puri ambaye nchi yake rais wa mzunguko kwenye chombo hicho ameelezea masikitio yake na kulaani juu ya mauwaji hayo ambayo ameyaita ya kuvunja moyo.