UM wasaidia Belize kupambana na HIV na Ukimwi

UM wasaidia Belize kupambana na HIV na Ukimwi

Shirika la maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP lina mpango wa kutekeleza makubaliono ya gharama ya dola milioni 3.1 na taifa Belize ili kutibu na kuzuia ugonjwa wa Ukimwi miongoni mwa vijana na watu wengine wazima kwenye taifa hilo lililo na idadi kubwa zaidi ya watu wanaoishi na virusi vya ukimwi kwenye eneo la Amerika ya kati.

Ufadhili huo unatolewa na shirika la Global Fund ambalo kwa sasa hivi limetoa dola bilioni 21.7 kwa nchi 150 kusaidia uzuiaji na matibabu ya ugonjwa wa Ukimwi. Shirika la Umoja wa Mataifa kupamba na ugonjwa wa Ukimwi UNAIDS linakadiria kuwa wa sasa watu 3600 wanaishi na virusi vya Ukimwi nchini Belize.