Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uchafuzi wa mazingira katika eneo la Ogoniland hatari kwa afya

Uchafuzi wa mazingira katika eneo la Ogoniland hatari kwa afya

Ripoti iliyotolewa hii leo na shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa inaonyesha kuwa uchafuzi wa mazingira unaosababishwa na mafuta katika eneo la Ogoniland nchini Nigeria umehatarisha zaidi afya ya binadamu. Ripoti hiyo inasema kuwa huenda ikachukua hadi miaka 30 kusafisha maeneo hayo yaliyochafuliwa.

Ripoti hiyo inaonyesha kuwa kiwango cha uchafuzi wa mazingira ni cha juu kuliko ilivyotarajiwa. Kwenye jamii moja maji ya kunywa yalichafuliwa pamoja na mito. Sasa ripoti hiyo inapendekeza kuwa serikali ya Nigeria pamoja na sekta ya mafuta wachange dola bilioni moja zitakazotumika kusafisha maji yaliyochafuliwa pamoja na ardhi.Mounkaila Goumandakoye ni mkurugenzi wa ofisi ya UNEP eneo hilo.

(SAUTI YA MOUNKAILA GOUMANDAKOYE)