Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM walaani matumizi ya nguvu dhidi ya raia nchini Syria

UM walaani matumizi ya nguvu dhidi ya raia nchini Syria

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limelaani ghasia zinazoendeshwa na serikali ya Syria dhidi ya raia . Kulingana na taarifa iliyotolewa na balozi wa India kwenye Umoja wa Mataifa Hardeep Sing Puri ni kuwa wanachama wa baraza hilo walitaka kusitishwa mara moja kwa ghasia nchini Syria.

Mamia ya watu wameuawa tangu kuanza kwa ghasia hizo. Mkuu wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa anasema ana ripoti kuwa waandamanaji 150 waliuawa wakati wa oparesheni ya serikali huku serikali ikidai kuwa wanajeshi 350 wameuawa na upande wa upinzani.