Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wabakaji lazima wakabiliwe na sheria sio maripota:UM

Wabakaji lazima wakabiliwe na sheria sio maripota:UM

Mjumbe maalum wa Katibu mkuu  wa Umoja wa Mataifa kuhusu dhuluma za kingono kwenye mizozo Margot Wallström ameelezea kusikitishwa kwake baada ya mahakama nchini Sudan kumfunga mwandishi mmoja wa habari aliyeripoti tukio ambapo mwanaharakati mmoja alibakwa na wanajeshi akisisitiza kuwa wahusika ndio wanastahili kufungwa na wala sio wanaoripoti.

Wallstrom amesema kuwa hukumu kama hizo sio tu zinaenda kinyume na haki ya kusema na vyombo vya habari bali zinawazuia waathiriwa wa dhuluma za kingono kusema hadharani uovu uliotendwa dhidi yao.