Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chombo cha kung’amua majanga kuanza kujaribiwa wiki ijayo

Chombo cha kung’amua majanga kuanza kujaribiwa wiki ijayo

Jaribio la kwanza kupima uwezo wa chombo kinazoweza kutambua uwezekano wa kutokezea janga la Tsunami linatazamiwa kufanywa wiki ijayo katika maeneo ya bahari ya Atlantic na Mediterranean.Chombo hicho ambacho kinaratibiwa na Umoja wa Mataifa ni cha kwanza kuwekwa kwenye eneo hilo kikiwa na shabaya ya kutoa ung’amuzi wa mapema uwezekano wa kutokea janga la tsunami.

Chombo cha ung’amuzi wa mapema juu ya uwezekano wa kutokezea majanga ya kimaumbile kilianzishwa mwaka 2005, chini ya uratibu wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na elimu, sayansi na utamaduni UNESCO.Jumla ya nchi 31 zimetajwa kuwa zitahusika kwenye jaribio hilo la kuweka ung;amuzi litakalofanywa wiki ijayo.