Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mjumbe wa UM aonya kuwa makabiliano kati ya wanajeshi wa Israel na Lebanon huenda yakaleta vita

Mjumbe wa UM aonya kuwa makabiliano kati ya wanajeshi wa Israel na Lebanon huenda yakaleta vita

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Lebanon Michael Williams amesema kuwa makabiliano ya risasi yaliyoshuhudiwa wiki hii kati ya wanajeshi wa Lebanon na wale wa Israel waliovuka eneo la Blue Line linalotenganisha nchi hizo mbili huenda yakaleta vita.

Akiongea alipokutana na waziri mkuu wa Lebanon Najib Mikati mjini Beirut Williams amesema kuwa makabiliano hayo yalikuwa tukio la kushangaza. Wawili hao pia walijadili suala la kushambuliwa kwa kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini Lebanon UNIFIL ambapo Williams ameitaka serikali ya Lebanon kuchukua hatua na kwafikisha mbele ya sheria wahusika.