Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wakaribisha vikwazo wa wale watakaokiuka haki za watoto Somalia

UM wakaribisha vikwazo wa wale watakaokiuka haki za watoto Somalia

Mjumbe maalum wa Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu watoto na mizozo Radhika Coomaraswamy amekaribisha uamuzi wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa baada ya kukubali kumwekea vikwazo yeyote ambaye atakiuka haki za watoto nchini Somalia.

Mjumbe huyo amesema kuwa ikiwa yeyote atamuua , kumuajiri , kumdhulumu kingono mtoto, au kama yeyote atashambulia shule au hospitali atakabiliwa na sheria akiongeza kuwa hii ni hatua mbele katika kumaliza ukwepaji wa sheria miongoni mwa wale wanaokiuka haki za watoto wakati wa vita.

Kati ya vikwazo ambavyo vitawekwa kwa yeyote ambaye atakiuka haki za watoto ni pamoja na vikwazo vya sialaha, vya kusafiri na kutwaliwa kwa mali. Mjumbe huyo ameyataka mashirika yanayohusika katika kuwalinda watoto kufanya jitihada na kupata habari za vitendo vya ukiukaji wa haki za watoto.